habari Mpya


Yanga Yaitungua Simba Ligi Kuu.

Kiungo mshambuliaji wa Yanga SC,Bernard Morrison leo March 8, 2020 ametenda kazi yake kwa kuifunga Simba SC bao 1-0 kwenye mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara 2019/2020 uliochezwa Uwanja wa Taifa.

 Bernard Morrison aliyefunga bao hilo pekee la ushindi dakika ya 44 kwa mpira wa adhabu alioupiga kiungo huyo raia wa Ghana na kuuzamisha mazima langoni baada ya Aishi Manula kuzidiwa nguvu na mpira huo.

Mchezo wa leo umehudhuriwa na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Ahmad Ahmad na Wenyekiti wa klabu zote, Dk. Mshindo Msolla wa Yanga SC na Mohamed ‘Mo’ Dewji wa Simba SC.   

Ushindi wa leo unaifanya Yanga SC kufikisha pointi 50 katika mchezo wa 25 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya tatu, sasa ikizidiwa pointi moja Azam FC inayoshika nafasi ya pili na point 51 ingawa mecheza mechi mbili zaidi.

Mabingwa watetezi, Simba SC wanaendelea kuongoza Ligi Kuu kwa mbali, wakiwa na pointi 68 baada ya kucheza mechi 27.

Post a Comment

0 Comments