habari Mpya


Wavuvi Waipongeza Serikali kuhusu Ongezeko la Samaki Ziwa Victoria.

Baadhi ya Wavuvi na wafanya biashara wa Samaki katika ziwa Victoria wameishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa juhudi ilizofanya za kudhibiti uvuvi usiokubalika na kusababisha ongezeko kubwa la Samaki.

Hayo yamesemwa na mwenyeki wa kikundi cha usimamizi wa rasilimali za uvuvi (BMU) katika mwalo wa Nyamikoma Bw. George James alipokuwa akizungumza mbele ya sekretarieti ya chama cha mapinduzi mkoa wa Simiyu ilipotembelea mwalo huo kwa lengo la kuwasikiliza wavuvi.


Hata hivyo ongezeko hilo la Samaki limefikia wastani wa tani 60 kwa mwezi ikilinganishwa na hapo awali ambapo walikuwa wakipata tani sita kwa mwezi hali iliyopelekea bei ya Samaki kushuka.

Aidha kwa upande wake katibu wa CCM mkoa wa Simiyu Bi. Haula Kachwamba amezungumzia mafanikio yaliyopatikana na kutoa msimamo wa chama cha mapinduzi katika ulinzi wa rasilimali za taifa.


Ziara hiyo ya sekretarieti ya CCM mkoa wa Simiyu ni sehemu ya kukagua utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi kwenye sekta ya uvuvi pamoja na kutathimini zoezi la oparesheni Sangara inayoendelea kufanywa na serikali katika ziwa victoria.

Post a Comment

0 Comments