habari Mpya


Muonekano wa Msikiti Mpya wa BAKWATA Jijini DSM Ujenzi Umefikia Asilimia 96.

Muonekano wa Msikiti ambao Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akiwa na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubeiry Bin Ally na Viongozi wengine waandamizi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) ametembelea na  kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Msikiti huo wa BAKWATA unaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohamed wa VI wa Morocco Kinondoni jijini Dar es salaam leo Ijumaa  Februari 28, 2020.

…Akiwa  na viongozi  waandamizi wa BAKWATA  akikagua maendeleo ya ujenzi wa msikiti huo.....

Msikiti huo unajengwa kwa ufadhili wa Mfalme Mohammed VI wa Morocco baada ya kuombwa na Rais Magufuli alipofanya ziara rasmi hapa nchini Oktoba 2016. 
 
Akiendelea  kukagua  baadhi ya sehemu za ujenzi huo. 

Rais Magufuli amejionea kazi za ukamilishaji wa jengo jipya la msikiti na jengo la ofisi ya Taasisi ya Mfalme Mohammed VI wa Morocco zikiendelea kukamilishwa na ameelezea kufurahishwa kwake na ubora na uzuri wa msikiti huo. 
…Akipita sehemu ambazo zimekamilika kujengwa.  

Rais Magufuli amemshukuru Mfalme Mohammed VI wa Morocco kwa kutekeleza ombi alilomuomba la kuwajengea Waislamu msikiti mkubwa kuliko yote hapa nchini, na amempongeza Mufti wa Tanzania na Waislamu wote kwa kujengewa nyumba nzuri ya ibada.

Mufti, Sheikh Aboubakar Zubeir bin Ally,  amemshukuru Rais Magufuli kwa kuwajali Waislamu na kuwaombea msaada wa kujengewa msikiti huo ambao ujenzi wake umefikia asilimia 96. 

Post a Comment

0 Comments