habari Mpya


Upungufu wa Madarasa 9,114 Waitesa Halmashauri ya Mji wa Kahama.

Na Juventus Juvinary –RK Kahama.

Idara ya Elimu Msingi katika Halmashauri ya mji wa Kahama mkoani Shinyanga inakabiliwa na upungufu wa vyumba vya madarasa elfu 9 na 114 ambavyo ujenzi wake unagharimu kiasi cha shilingi bilioni 54.

Afisa elimu wa shule za msingi katika halmashauri ya mji wa Kahama Bw. Aluko Lukolela ameiambia Radio Kwizera kuwa ujenzi wa miundombinu hiyo hauwezi kutekelezwa na halmashauri pekee hivyo, ni jukumu la wazazi na walezi wenye watoto na jamii yote kujitolea.

Kuokana na hali hiyo, ametoa wito kwa viongzi wa serikali za mitaa kuhimiza jamii kujitolea kujenga vyumba vya madarasa hadi usawa wa Renta, na halmashauri itamalizia uekezaji na kutoa samani pamoja na vifaa vya kufundishia.
Kadhalika Afisa Elimu Aluko Lukolela amesema wachangiaji si lazima watoe fedha tu, bali hata mali zinazoweza kuthaminishwa kwa fedha.

Post a Comment

0 Comments