habari Mpya


Simba SC na Mtibwa Sugar Fainali January 13, Kombe la Mapinduzi 2020.

Golikipa Beno David Kakolanya akipongezwa na wachezaji wenzake wa Simba SC baada ya kupangua penati ya mwisho ya Azam FC na kuipeleka Simba SC fainali ya Kombe la Mapinduzi 2020 kwa ushindi wa penati 3-2 baada ya sare 0-0 usiku wa jana January 10,2020 kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Kakolanya aliye katika msimu wake wa kwanza Simba SC, tangu awasili kutoka kwa mahasimu, Yanga alipangua penati ya kipa mwenzake, Mghana Razack Abalora.

Awali Abalora aliokoa penati mbili za Simba SC, ya kwanza ya kiungo wa kimataifa wa Sudan, Sharaf Eldin Shiboub na baadaye ya mshambulaji wa kimataifa wa Rwanda, Meddie Kagere.

Sasa Simba SC itakutana na Mtibwa Sugar ya Morogoro katika fainali January 13,2020 ambayo iliitoa Yanga kwa penati 4-2 baada ya sare ya 1-1.

Post a Comment

0 Comments