habari Mpya


Simba SC na Azam FC Nusu Fainali Kombe la Mapinduzi 2020 January 10.

Wekundu wa Msimbazi Simba SC watavaana na Azam FC katika nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi 2020 siku ya Ijumaa January 10,Uwanja wa Amaan, Zanzibar kuanzia Saa 2:15 usiku.

 Simba SC ambao ni Mabingwa wa Tanzania Bara,wameenda hatua hiyo wakiwaondosha Timu ya Zimamoto ya Zanzibar kwa kuwachapa mabao 3-1 jioni ya January 7,2020 Uwanja wa Gombani, Pemba.

Mabao ya Simba SC yamefungwa na Nahodha wake, John Bocco dakika ya 5 na viungo, Msudan Sharaf Eldin Shiboub dakika ya 9 na mzawa, Ibrahim Ajibu dakika ya 54, wakati bao pekee la Zimamoto limefungwa na Ibrahim Ahmad ‘Hilika’ dakika ya 29.

Azam FC yenyewe ilitangulia nusu fainali baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Mlandege SC, kwa bao pekee la mshambuliaji wake Mzambia, Obrey Chirwa dakika ya 57.

Nusu Fainali hiyo itakuwa sawa na marudio ya fainali ya michuano hiyo mwaka 2019 Uwanja wa Gombani, ambayo Azam FC iliibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Simba SC wakati huo ikiwa chini ya kocha mwingine Mbelgiji, Patrick Aussems aliyefukuzwa Desemba 2019.

Post a Comment

0 Comments