habari Mpya


RC Kagera Aridhishwa na Kasi ya Ujenzi wa Miradi 9 ya Maendeleo wilayani Ngara.

Ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti kutembelea na kukagua Mradi wa kufua umeme unaotekelezwa kwa fedha kutoka  Benki ya Dunia zaidi ya Dola za Kimarekani Milioni 340 huku Benki ya Afrika ikifadhili ujenzi wa laini ya umeme huo Kwa Nchi tatu za Rwanda, Burundi na Tanzania.

Kukamilika kwa mradi huo wenye uwezo wa kutoa Megawati 80 kutazifanya Nchi hizo tatu kunufaika na Umeme wa Megawati 27 kila Nchi Mwanachama.
Pichani juu na chini ni  Ujenzi wa Intack Gate , Power House na Switch Yard Ukiendelea kwenye Maendeleo ya Mradi wa Kufua Umeme wa Rusumo unaoziunganisha nchi tatu za Tanzania  , Burundi na Rwanda. 
Katika Hatua nyingine,Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti ameridhishwa na maendeleo ya mradi wa maendeleo Vijijini (LADP) unaotekelezwa na Halmashauri ya Wilaya ya Ngara mkoani Kagera na kusimamiwa na NELSAP, mradi wenye thamani ya shilingi bilioni 11 na milioni 400.

Amesema ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa miradi 9 ikiwemo ya Zahanati ya Rusumo, Bweni la Wasichana, Madarasa matano, Jengo la utawala na nyumba ya mwalimu Shule ya msingi Makungwa, ujenzi wa miundombinu katika kituo cha Afya Lukole miradi ambayo mpaka sasa imegharibu shilingi bilioni 2.6.

Aidha amewataka wakandarasi wote wanaosimamia miradi hiyo kuikamilisha kwa wakati ili wananchi waweze kuanza kunufaika nayo.

Brigedia Jenerali Marco Gaguti amekuwa kwenye ziara ya siku mblii wilayani Ngara ya kukagua miradi ya maendeleo inayojengwa katika Halmashauri ya wilaya hiyo ambapo January 16,2020 alikagua mradi wa kufua umeme wa maporomoko ya Rusumo. 
 

Post a Comment

0 Comments