habari Mpya


Mume Amuuwa Mkewe Wakigombea Nyumba Wilayani Kibondo.

Na James Jovin –RK Kibondo.

Mwanaume mkazi wa Kibondo mjini mkoani Kigoma amemuua mke wake kwa kumpiga na kitu chenye ncha kali kichwani kutokana na ugomvi wa kugombania mali.

Tukio hilo limetokea January 12, 2020, majira ya mchana ambapo mwanaume Albert Rugai alimuuwa mkewe Estha Kondo baada ya kutokea ubishi kati yake na mkewe wakiwa wanagombania nyumba waliyojenga, mwanaume akihitaji hati iandikwe kwa jina lake.

Akizungumza na Redio Kwizera, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya wilaya ya Kibondo Dr. Mathias Bwashi amesema kuwa walipokea mwili wa marehemu Jumapili majira ya saa mbili za usiku pamoja na mume wake aliyekuwa akitokwa povu mdomoni kwa kuwa alitaka kujinyonga na kisha kumfanyia matibabu.
Jeshi la Polisi wilayani Kibondo limethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba uchunguzi zaidi wa tukio hilo unaendelea na kwa sasa wamemshikilia mtuhumiwa Albert Rugai.

Post a Comment

0 Comments