habari Mpya


Maafisa Maendeleo ya Jamii Toeni Elimu ya Lishe Nchini - Dkt. Ndugulile.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, JInsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akikoroga uji kwa ajili ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Myigumba iliyopo mkoani Iringa wakati wa ziara yake Shuleni hapo kuangalia masuala ya Lishe.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akipanda mbegu ya mahindi katika shamba la Shule ya Msingi Mnyigumba iliyopo Rungemba mkoani Iringa wakati wa ziara yake Shuleni hapo kuangalia masuala ya Lishe.

Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, JInsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amewataka Maafisa Maendeleo ya Jamii kuweke mkazo kwa kutoa elimu ya lishe nchini hasa katika shule za misingi na Sekondari nchini ili kuondokana na tatizo la udumavu na utapiamlo.

Ameyasema hayo January 8,2020 mkoani Iringa alipotembela Shule ya msingi Mnyigumba ambapo shule hiyo imelima shamba kwa ajli ya mahindi lishe yatakayosaidia kuwapatia mlo wa asubuhi na mchana wanafunzi.

Ameongeza kuwa Sera ya elimu bure ina maana ya kuwa wazazi na walezi kutochangia katika kuhakikisha wananfunzi wanapata chakula wakati wakiwa shleni ili kuhakikisha wanazingatia masomo yao na kuongeza ufaulu.

Elimu bure sio sababu ya wazazi, walimu na shule kutokuwa wabunifu katika kuhakikisha wanajiongeza katika masuala ambayo yatasaidia wanafunzi kuongeza juhudi katika masomo na kuongeza ufaulu”alisema Dkt. Ndugulile.

Amesisitiza kuwa elimu ya lishe inatakiwa kutolewa kwa wananchi hasa katika maeneo ambayo tatizo la udumavu na utapiamlo linaongezeka kwa kasi katika maeneo ya Nyanda za juu kusini ikiwemo mkoa wa Iringa ingawa mikoa hiyo inaogoza katika uzalishaji chakula nchini.

Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Msingi Mnyigumba Bw. Richius Mwamanga amesema kuwa Shule imelima shamba la mahindi lililozalisha jumla ya kilo zilizosaidia kutoa chakula kwa wnaanfunzi wa shule hiyo hivyo kusaidia wanafunzi hao kuzingatia masomo na kuongeza ufaulu wao.

Post a Comment

0 Comments