habari Mpya


Bilioni 5 zinatumika Kufanya Matengenezo Barabara ya Lusahunga hadi Rusumo mkoani Kagera.

Muonekano wa sasa wa eneo la Nyabugombe katika Barabara ya Lusahunga hadi Rusumo ambayo inaunganisha nchi za Burundi na Rwanda imekuwa ikisababisha hasara na madhira mengi kwa wasafiri ambapo January 29 mwaka huu2020, zaidi ya Magari 300 yakiwemo ya mizigo na ya abiria yalikwama kwa tabriban saa12 katika eneo la Nyabugombe na kusababisha usumbufu kwa wasafiri.

Kwa sasa Jumla ya shilingi bilioni Tano zinatumika kwa ajili ya kufanya matengenezo ya barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 91 ikiwemo matengenezo ya kawaida, matengenezo ya muda maalum na matengenezo ya maeneo karofi ikiwemo eneo la Nyabugombe ambalo limekuwa likisababisha mkwamo wa magari mara kwa mara. 

Akizungumza kwa njia ya simu na radio Kwizera akiwa manispaa ya Bukoba, Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Mkoa wa Kagera Mhandisi Adrea Kasamwa amesema kwa sasa usanifu wa barabara hiyo ya Lusahunga hadi Rusumo umekamilika, na kinachosubiriwa ni fedha nyingine ili ianze rasmi kukarabatiwa kwa kiwango cha lami.

Katika kufuatilia ni kwa namna gani barabara hiyo itafanyiwa matengenezo ili kurahisisha usafiri, mwana habari wetu Mohamed Ramadhan Makonda ameongea hapa chini na Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Mkoa wa Kagera Mhandisi Adrea Kasamwa, na kwanza amemuuliza nini TANROADS Kagera inakifanya katika kutengeneza barabara hiyo?


BOFYA HAPA  CHINI KUSIKILIZA ZAIDI. 

Eneo hilo ni sehemu ya Barabara kutokaa Lusahunga hadi Rusumo ambayo inaunganisha nchi za Burundi na Rwanda ambayo imekuwa ikisababisha kukwama kwa magari mara kwa mara kutokana na ubovu uliopo kwenye barabara hiyo.

Post a Comment

0 Comments