habari Mpya


Wanakagera Watakiwa kutoa Ushirikiano kwa Jeshi la Polisi Kagera.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, ACP Revocatus Malimi. 
 
Na Anord Kailembo -RK Bukoba.

Jeshi polisi Mkoani Kagera limewataka wakazi mkoani humo kujenga tabia ya kutoa taarifa za mapema pindi wanapobaini uwepo wa viashiria vya uvunjifu wa amani kwenye maeneo yao ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza.

Kamanda wa jeshi la polisi Mkoani Kagera Bw.Revocatus Malimi amesema jeshi la polisi linategemea kwa kiasi kikubwa ushirikiano wa wananchi kutekeleza majukumu yao kwani ni vigumu kutambua maeneo yanayohitaji msaada wa jeshi hilo iwapo wananchi wenyewe hawatatoa taarifa.
Amesema jeshi hilo limejipanga kuhakikisha wananchi wa mkoa wa Kagera wanafanya shughuli zao katika hali ya usalama na kwamba bado upo uhitaji mkubwa wa kuwepo kwa ulinzi shirikishi kuanzia ngazi ya mitaa na vijiji.
Nao Baadhi ya Wakazi wa Manispaa ya Bukoba, wamesema jeshi linatakiwa kuimarisha mahusiano yao na wananchi kwani bado ipo hali ya wananchi kuliogopa jeshi hilo lakini pia kuhofia usalama wao baada ya kutoa taarifa za uharifu kwa jeshi hilo.

Post a Comment

0 Comments