habari Mpya


Waliochaguliwa Kujiunga na Kidato cha Kwanza Mwaka 2020.

Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI, Mhe. Selemani Jafo ametangaza wanafunzi waliochaguliwa kujiunga  na Kidato cha Kwanza  mwaka 2020  kuwa ni  701,038 sawa na asilimia 92.27 ya wanafunzi 759,000 waliofaulu.


Mhe Jafo ameeleza kuwa wavulana waliochaguliwa ni 335,513 sawa na asilimia 47.86 na wasichana 365,525 sawa na asilimia 52.14.Mhe. Jafo alifafanua kuwa kwa mwaka 2019 jumla ya wanafunzi 759,737 walifaulu sawa na asilimia 81.3 ya waliofanya mtihani, wakiwemo wavulana 363,999 sawa na asilimia 47.9 na wasichana 395,738 sawa na asilimia 52.08.Kati ya waliofaulu wamo wanafunzi wenye Ulemavu 1,461 sawa na asilimia 0.19 wakiwemo wavulana 777 na wasichana 684 aliongeza Jafo.

Post a Comment

0 Comments