habari Mpya


Sekta ya Nishati Nchini Inatajwa kuwa na Mchango Mkubwa Kuleta Usawa wa Kijinsia ikiwa Vyombo vya Habari na Wadau wataipa Kipaumbele.

Baadhi ya Wakufunzi na Waandishi wa habari wanaoshiriki katika mafunzo ya nishati jadidifu.

Na Aurelia Gabriel –RK Dar Es Salaam.

Sekta ya Nishati nchini inatajwa kuwa na mchango mkubwa kuleta usawa wa kijinsia ikiwa vyombo vya habari na wadau mbalimbali wataipa kipaumbele kwa kutoa taarifa za kina juu ya matumizi ya Nishati jadidifu.

Ni kauli yake Bw. Thabit Mikidadi, Afisa mawasiliano kutoka mtandao wa Nishati na Jinsia Tanzania TANGSEN wakati akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari juu ya kuripoti taarifa za Nishati na usawa wa kijinsia jijini Dar es salaam.

Bw. Mikidadi anasema kwa sasa mwanamke bado anaonekana kuwa chini hasa katika sekta ya uchumi kutokana na ukosefu wa nishati muhimu inayoweza kumkomboa.
Jumla ya waandishi wa habari 20 kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini Tanzania ikiwemo Radio Kwizera, wamepatiwa mafunzo kwa vitendo juu ya namna ya kuandaa na kuripoti habari za Nishati jadidifu, mafunzo yanatolewa na kampuni ya habari na teknolojia ya NUKTA AFRIKA kwa ushirikiano na chama cha waandishi wa Mazingira Tanzania JET yaliyoanza Disemba 10 na kuhitimishwa Disemba 14 mwaka huu,2019 jijini Dar es salaam.

Nishati Jadidifu ni nishati mbadala inayozalisha umeme itokanayo na vyanzo asilia kama vile mwanga wa jua, nguvu ya upepo, kinyesi, maji na joto kutoka ardhini na hudumu kwa muda mrefu.

Post a Comment

0 Comments