habari Mpya


Kilimanjaro Stars Yahitaji Ushindi Jumamosi ili kwenda Nusu Fainali Cecafa.

Bao pekee la dakika ya 38  la Ditram Nchimbi  limeiwezesha Timu ya Kilimanjaro Stars  kushida mchezo wake wa kwanza mbele ya Zanzibar Heroes kwenye michuano ya Afrika Mashariki na Kati (Cecafa).


Mchezo wa kwanza wa ufunguzi Kilimanjaro Stars ilipoteza kwa kuchapwa bao 1-0 na Kenya lililopachikwa dakika ya nne.

Katika Michuano hiyo inayofanyika nchini Uganda , kwenye mchezo mwingine Kenya amabo ndiyo mabingwa watetezi wa michuano hiyo, tayari wameenda nusu fainali baada ya kushinda 2-1 dhidi ya Sudan katika mchezo wa kwanza.  

Licha ya Ushindi,Kilimanjaro Stars itahitaji ushindi katika mechi ya mwisho Jumamosi December 14,2019 dhidi ya Sudan ili kwenda Nusu Fainali.

Post a Comment

0 Comments