habari Mpya


Polisi Kagera Waua Majambazi Wanne.

Na Anord Kailembo –RK Bukoba.

Oparesheni maalum inayoendeshwa na jeshi la polisi kwenye maeneo korofi hasa kwenye mapori ya mikoa ya Kigoma, Kagera na Geita imefanikisha kuuawa kwa wata wanne wanaotuhumiwa kuwa ni majambazi katika pori la Biharamulo na baada ya kukaguliwa wamekutwa na Bunduki ya Ak 47 na Magazine yenye risasi 7.

 Kamishina wa polisi, oparesheni na mafunzo Riberatus Sabasi akizungumza na vyombo vya habari ameeleza kwamba usiku wa kuamkia jana askari wa oparesheni hiyo wakiwa katika doria kwenye barabara kuu ya kuelekea Nchini Rwanda na Burundi walishuhudia kundi la watu likitokea polisi na walivyotakiwa kujisalimisha wakaanza kuwashambulia askari.

Amesema kuwa, wakati wakijibizana kwa risasi wanne kati yao waliuawa na wengine wakatokomea kusikojulikana ambapo wanaendelea kutafutwa.

Aidha Kamishina Sabasi amesema kuwa oparesheni iliyoendeshwa wilayani Kasulu imewakamata watu 42 kwa makosa mbalimbali na kati yao, 24 wakihusika na matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha huku wakikiri kuhusika katika matukio mbalimbali

Post a Comment

0 Comments