habari Mpya


Wanafunzi 1826 Kuhitimu Elimu ya Kidato cha Nne Wilayani Kibondo.

Na James Jovin –RK Kibondo.

Jumla ya wanafunzi  elfu moja ,mia nane na 26, wanatarajia kuhitimu elimu ya kidato cha nne, wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma. 

Akizungumza na Redio Kwizera akiwa Ofisini kwake, Kaimu Afisa Elimu wa Shule za Sekondari Wilayani Kibondo, Bw. Salvatory Gwiboha  amesema Watahiniwa wa Kike ni  8,41 na  Wakiume ni 9,72 na watafanya Mtihani huo kuanzia November, 4 mwaka huu,2019.
Bw. Gwiboha amesema kuwa maandalizi ya mtihani huo kwa wilaya ya Kibondo yanaendelea vizuri na tathmini iliyofanyika inaonesha kiwango cha taalumu katika wilaya ya Kibondo kinaendelea kupanda. 

Katika hatua nyingine amewataka wazazi na walezi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Vijana wao na kuwapa vifaa vinavyohitajika katika mitihani ili waweze kufanya vyema mtihani huo.
Nao Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Misezero, wamejigamba kufanya vyema mtihani huo kwani wamejiandaa vizuri licha ya changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo  ukosefu wa madawati pamoja na maabaara  kwa ajili ya masomo ya sayansi.

Post a Comment

0 Comments