habari Mpya


Tanzania yaenda (CHAN) 2020 Kibabe.

Tanzania imefanikiwa kukata tiketi ya kucheza Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) mwakani 2020 nchini Cameroon baada ya ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya wenyeji, Sudan October 18, 2019 mjini Omdurman.

 Shujaa wa Tanzania katika mchezo huo, alikuwa ni mshambuliaji Ditram Nchimbi akifunga bao la pili huku Erasto Edward Nyoni akaenda kufunga kwa shuti la mpira wa adhabu dakika ya 49 kuisawazishia Taifa Stars.

Kwa matokeo hayo, Taifa Stars inayofundishwa na kocha Mrundi, Etienne Ndayiragijje inafuzu CHAN ya 2020 kwa faida ya mabao ya ugenini baada ya sare ya jumla ya magoli 2-2, kufuatia kufungwa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza jijini Dar es Salaam.

Hiyo inakuwa mara ya pili kwa Taifa Stars kufuzu fainali za michuano hiyo inayoshirikisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee, baada ya mwaka 2009 nchini Ivory Coast, ikiitoa Sudan pia katika raundi ya mwisho ya kufuzu.

Sudan ilitangulia kwa bao la Amir Kamal dakika ya 30 akimalizia krosi ya Ahmed Adam Mohamed aliyemlamba chenga beki wa kulia wa Tanzania, Salum Kimenya.

Post a Comment

0 Comments