habari Mpya


Taarifa ya Mtoto wa Miaka 10 Kujifungua Shinyanga ni Uongo –Dr. Mfaume.

Na Amos John –RK Shinyanga 89.7


Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dr.Rashidi Mfaume amekanusha uwepo wa taarifa za mototo mwenye umri wa miaka kumi kujifungua katika hospitali ya wilaya yaShinyanga

Akizungumza na Waandishi wa habari Dr.Mfaume amefafanua kuwa uongozi wa idara ya afya ngazi ya mkoa umefanya ufuatiliaji katika vituo vyote vya afya na hospitali na kubaini kuwa hakuna mototo yeyote aliye jifungua mkoani humo

Aidha amewataka watu wanaoweka picha na matukio mtandaoni kufanya uchunguzi na ufuatiliaji kabla ya kuandika maana kufanya hivyo ni kupotosha jamii na kuchafua idara ya afya mkoani Shinyanga.

Mganga mkuu huyo wa mkoa amesisitiza kwamba hatua za kufuatilia muhusika aliyesambaza habari hizo zinaendelea ili hatua kali ziweze kuchukuliwa dhidi yake.

Post a Comment

0 Comments