habari Mpya


Soma Taarifa ya Habari Saa 24 Radio Kwizera FM.

Source; RK: AE (Serikali Uvinza kuchukua)
ED: AG
Date: Monday, October 21, 2019

UVINZA

Serikali wilayani Uvinza mkoani Kigoma imeahidi kuwachukulia hatua za kisheria wazazi na walezi watakaobainika kuwatumikisha watoto wao katika shughuli za kilimo na kusababisha kuwa watoro shuleni

Mkuu wa wilaya ya Uvinza Bi. Mwanamvua Mrindoko ameiambia Radio Kwizera kwamba unapofika msimu wa kilimo, baadhi ya wazazi na walezi wamekuwa wakiwatumikisha watoto wao katika shughuli za kilimo badala ya kuwahimiza kusoma

Aidha amesema serikali wilayani humo inatarajia kuanza msako wa nyumba kwa nyumba kwa lengo la kubaini watoto wasiohudhuria masomo darasani kwa sababu za kilimo ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa kwa wahusika

Kwa upabde wao baadhi ya wananchi wilayani Uvinza wamesema tatizo la kuwatumikisha watoto katika shughuli za kilimo kwa wilaya hiyo limekuwa sugu na kwamba serikali haina budi kuchukua hatua kwa wazazi na walezi watakaobainika kufanya hivyo.Source; RK: Elias Z (maliasili)
ED: AG
Date: Monday, October 21, 2019

CHATO

Serikali kupitia idara ya mali ya asili na utalii wilayani Chato mkoani Geita imewataka wananchi wanaopakana na hifadhi ya taifa Burigi kudumisha dhana ya ujirani mwema kwa kutoharibu mali za asili zilizopo ndani ya hifadhi hiyo ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa zinazoashhiria ujangili katika hifadhi hiyo.

Kauli hiyo imetolewa na mhifadhi Letisia Magesa wakati akiongea na wakazi wa kata ya Bwongera wilayani humo juu ya namna wanavotakiwa kudumisha ujirani mwema baina yao na hifadhi ya Taifa Burigi Chato.

Mhifadhi Letisia amesemo moja ya njia za kudumisha ujirani mwema ni pamoja na kutoa taarifa za siri zinazoashiria uharibifu wa maliasili katika hifadhi hiyo kama vile ujangili
Baadhi ya wakazi wa Bwongera wilayani Chato ambao wanapakana na hifadhi ya Taifa Burigi Chato wamesema wako tayari kulinda hifadhi hiyo kwa kutoa taarifa za ujangiri na wizi wawanyama pori endapo watabaini au kuona uwepo wa hali hiyo.

Source; RK: em (Mahakamani)
ED: AG
Date: Monday, October 21, 2019

KARAGWE

Mahakama ya wilaya ya Karagwe imewahukumu kifungo cha miaka 30 gerezani watu wawili baada ya kukutwa na kosa la kubaka na kulawiti

Mwendesha mashitaka wa jeshi la polisi wilaya ya Karagwe Bw. David Lomela mbele ya hakimu wa mahakama hiyo Bw. Michal Manjale amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Shukuru Hassan na Maganga Onesmo wakazi wa wilaya ya Kyerwa

Bw. Lomelo amesema kuwa mnamo Mei 22 mwaka huu, Maganga Onesmo alimlawiti mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 10 na Shukuru Hassan Januari 04 mwaka huu alimbaka mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 8 na  ametakiwa kumlipa faini mtoto aliyetendewa unyama huo kiasi cha shilingi laki nane

Awali mwendesha mashitaka kutoka jeshi la polisi ameomba mahakama iwapatie adhabu kali watuhumiwa hao ili kuwa fundisho kwa watu wengine


Source; Mwananchi AG (MARUFUKU)
ED: AG
Date: Monday, October 21, 2019

TANGA

Waziri wa Ardhi nchini William Lukuvi amepiga marufuku maofisa ardhi kutoa ofa ya viwanja kuanzia October 22,2019.

Akizungumza October 22,2019 na wananchi wa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga, Lukuvi amesema kwa sasa hakuna ofa itakayotolewa na Serikali.

Waziri Lukuvi amesema madhara yaliyojitokeza katika kutoa ofa ni kufanyika udanganyifu kwa watumishi wasio waaminifu na kuisababishia Serikali hasara.

Pia,  amesema masjala ya ardhi iliyokuwa mjini Moshi itahamia mkoani Tanga kwa sababu ni gharama kwa mwananchi kwenda Moshi kusaini hati kwa kuwa wengi hutumia gharama kubwa kufika katika mji huo wakati kiasi wanachotoa kwa ajili ya hati ni kidogo.

Vile vile ameridhia kuanzishwa kwa baraza la ardhi Handeni baada ya kuonyeshwa jengo na kuridhika nalo.


Source; Mwananchi: AG  (uchaguzi CCM)
ED: AG
Date: Monday, October 21, 2019
DAR ES SALAAM

Katibu mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally ameagiza kurudiwa kwa uchaguzi wa wagombea uongozi wa serikali za mitaa ndani ya chama hicho katika maeneo yaliyolalamikiwa nchi nzima kwamba yamekiuka kanuni za uchaguzi huo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ndogo za makao makuu ya chama hicho Lumumba jijini Dar es Salaam jana, Dk Bashiru pia ametaka mkoa wa Dar es Salaam urudie kazi hiyo ili kuhakiki mchakato wa uchaguzi.
Amesema yapo maeneo hawakufuata kanuni, na katika baadhi ya maeneo hayo kumekuwa na mgongano kiasi cha wanachama kususa kupiga kura

Mnamo Octoba 20 kwaka huu CCM ilifanya uteuzi wa ndani ili kupata wagombea kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa uliopangwa kufanyika Novemba 24 nchi nzima.

Post a Comment

0 Comments