habari Mpya


Soma Habari ya 24 October 03,2019 Radio Kwizera FM.

Source; RK: EE (Ebola)
ED: LG
Date: Thursday, October 3, 2019
NGARA
Wananchi wilayani Ngara mkoani Kagera wametakiwa kuendelea kuchukua tahadhari za kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Ebola ili kudhibiti ugonjwa huo kuingia nchini.

Mwenyekiti wa kamati ya wilaya ya kudhibiti Ebola ambaye ni mkuu wa wilaya ya Ngara Luten Kanali Michael Mtenjele kupitia kikao kazi cha kamati hiyo amesema licha ya kwamba Ugonjwa huo bado haujaingia nchini wananchi wanapaswa kuchukua tahadhari ikiwemo kuepuka kushikana mikono wakati wa kusalimiana.

Luten Kanali Mtenjele amewataka watendaji wa serikali na viongozi wa Dini kutumia mikutano na wakati wa Ibada kuelimisha jamii namna bora ya kuendelea kujikinga na ugonjwa huo.


Kwaupande wake Afisa Afya wa Wilaya Bw.Salum Kimbau amesema idara ya afya tayari imejiandaa kikamilifu na kwamba iwapo wananchi watamuona mtu mwenye dalili za ugonjwa wa ebola watoe taarifa kwa uongozi wa eneo husika ili wataalam watoe msaada wa haraka.

Source; RK: EZ (Mimba)
ED: LG
Date: Thursday, October 3, 2019
CHATO

Jeshi la polisi wilayani Chato mkoani Geita kupitia kitengo cha dawati la jinsia limeanza kutekeleza mkakati wa kutembelea shule za sekondari na msingi kuwaelimisha watoto wakike namna ya kukabiliana na mimba za utotoni.
Akiongea na kipindi hiki mkaguzi msaidizi wa Dawati la jinsia Bi.Stella Thomas amesema mpango huo ni wa muda mrefu nakwamba wamekusudia kutembelea shule zote zilizopo wilayani humo ili kuwajengea uwezo watoto wakike kujitambua hali itakayo saidia kuepuka mimba za utotoni.

Bi.Stella amesema jeshi la polisi wilayani humo kupitia dawati la jinsia halitomfumbia macho mwanaume yeyote atakaebainika kukatisha ndoto za mtoto wakikie kwa kumsababishia ujauzi.


Kwaupande wake Mkuu wa shule ya sekondari Buzilayombo Bw.Mussa Maganga amelipongeza Jeshi la polisi wilayani Chato kupitia dawati la jinsia kwa kuanza kushirikiana na walimu na wazazi kutoa elimu kwa watoto wao wa kike jambo ambalo amesema huwenda likasaidia kupunguza tatizo la mimba shuleni.


Source; RK: AE (Nidham)
ED: LG
Date: Thursday, October 3, 2019
KIGOMA

Mkuu wa mkoa wa Kigoma Brigedia Generali mstaafu Emmanuel Maganga amewataka watumishi wa serikali mkoani humo kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha ya serikali ili kuchochea maendeleo katika jamii.
Ametoa rai hiyo kufuatia afisa biashara wa manispaa ya Kigoma Ujiji Bw.Elija Ben Semfuko kutuhumiwa kwa ubadhilifu wa fedha ya vitambulisho vya wajasiliamali kiasi cha shilingi milioni 7na elfu 40.
Brigedia Generali Mstaafu Maganga amesema serikali haitasita kuchukua hatua kwa watumishi wa serikali wanaoshindwa kuzingatia sheria na kwamba hakuna anayeruhusiwa kutumia fedha za serikali bila kufuata utaratibu wa kisheria.


Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kigoma Bw.Samson Anga amesema zoezi la ugawaji wa vitambulisho vya wajasiliamali katika wilaya hiyo linaendelea vizuri na kwamba jumla ya vitambulisho 261 moja vyenye thamani ya shilingi milioni 5 laki 2 na elfu 20 vimesha chukuliwa. 

Source; RK: FM (Mimba)
ED: LG
Date: Thursday, October 3, 2019
SHINYANGA
Jumla ya wanafunzi sabini na moja wilaya ya Shinyanga vijijini mkoani Shinyanga wamekatiza masomo yao baada ya kupata ujauzito kwa kipindi cha mwezi Julai mwaka jana hadi June mwaka huu.
Hayo yameelezwa na Afisa Maendeleo ya jamii wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga vijijini Bw.Deusi Mhoja alipokuwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya siku ya wazee duniani ambayo kiwilaya yamefanyika kata ya Tinde wilaya ya Shinyanga vijijini

Bw.Mhoja amesema kati ya wanafunzi hao waliopata ujauzito 6 ni wanafunzi wa shule za msingi huku wanafunzi sitini na tano wakiwa ni wa shule za secondary nakwamba ipo haja kwa jamii kuungana na serikali kupinga vitendo hivyo

Kwa upande wake katibu wa baraza la wazee wa halmashauri hiyo Bw.Boniphace Boazi amesema katika kuadhimisha siku hiyo bado kundi la wazee linaonekana kuachwa nyuma katika huduma mbalimbali za kijamii hivyo serikali inapaswa kulitazama upya suala hilo.

Source; RK: WM (Shule)
ED: LG
Date: Thursday, October 3, 2019
BIHARAMULO
Baadhi ya wakazi wa kitongoji cha Nyakahama na Muungano kata ya Lusahunga wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera wameiomba serikali kusajili shule shikizi ya Muungano iliyoanzishwa na wananchi zaidi ya miaka 9 iliyopita.
Wananchi hao wamesema  changamoto ya watoto wao kutembea umbali mrefu  kwenda shule ya msingi Nyambale na Nyamaragara imepelekea wananchi kujenga madarasa mawili  ya yanayotumiwa na wanafunzi wa darasa la kwanza hadi la nne ili kukabiliana na tatizo la watoto kushindwa kuendelea na masomo kutokana na umbali.
Mwalimu wa kujitolea  wa shule shikizi ya Muungano  Bw.George  Samusoni  amesema   shule hiyo ina wanafunzi zaidi 300  wa darasa la kwanza hadi la nne ambao walikuwa  wakitembea umbali wa kilometa 10 hadi 12  kwenda shule  mama ya Nyambale na  Nyamaragara  ambapo kwasasa wanaenda katika shule hizo kwaajili ya kuungana na wenzao kufanya mtihani wa kimkoa na kitaifa.
Naye kaimu  afisa elimu  msingi  Wilaya ya  Biharamulo  Bw. Idd  Mrisho  amesema hajapata  taarifa  rasmi juu ya shule hiyo  na kuahidi  kufuatilia  ili kuangalia uwezekana wa kuisajili ili kunusuru  wanafunzi wanaotembea  umbali mrefu.


Source; RK: JJ (Majeruhi)
ED: LG
Date: Thursday, October 3, 2019
NGARA

Mfanyabiashara mmoja Bw.Eugen Philip makazi wa mamlaka ya Mji Mdogo wa Rulenge wilayani Ngara amelazwa Hospitali ya Kristo mfalme Rulenge akipatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa na watu wanao dhaniwa kuwa majambazi walio mvamia nyumbani kwake.

Akizungumza na Radio Kwizera katika Hospitali hiyo ya Kristo mfalme Bw.Eugen Philip amesema tukio hilo limetokea Saa 8 usiku wa kuamkia leo nakwamba watu hao wamempora fedha na Vocha za Simu zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 47.

Aidha Daktari aliye mpokea majeruhi huyo Dakt.Godian Beyanga amesema mgonjwa amejeruhi kwa kupigwa na kituchenye ncha kali sehemu za Shingoni, mikononi na Mdomoni nakwamba baada ya kumpatia matibabu kwasasa hali yake inaendelea vizuri.
Hata hivyo Polisi wilayani Ngara wamefikak eneo la tukio na wanaendelea na msako ili kuwabaini walio husika na tukio hilo.

Source; RK: SM (Chanjo)
ED: LG
Date: Thursday, October 3, 2019
KIBONDO

Jumla ya kiasi cha Shilingi Milioni Arobaini na tisa na laki nne kimetengwa kwa ajili ya zoezi la kuendesha kampeni ya kutoa chanjo ya Polio, Surua Lubella kwa watoto walio chini ya miaka mitano Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma.
Mganga Mkuu wa hosipitali ya wilaya ya Kibondo Dakt.Sebastian Pima amesema zoezi hilo linatarajia kuanza Octoba 15 hadi 19 mwaka huu ili kuwakinga watoto dhidi ya magonjwa hayo.
Amesema magonjwa hayo hayana tiba bali watoa huduma hutibu matokeo ya ugonjwa huo ambayo ni upele kuanzia kwenye uso, kutokwa na usaha masikioni, homa na vichomi, hivyo jamii inatakiwa kuliwekea mkazo suala hilo.Naye Mkurugenzi mtendaji wa halmshauri ya wilaya ya Kibondo Bw. Deoclas Lutema akimwakilisha Mkuu wa Wilaya amesema mikakati iliyojadiliwa kupitia kikao hicho endapo itafanyiwa kazi, itasaidia kutokomeza ugonjwa huo.

Post a Comment

0 Comments