habari Mpya


RC Katavi Atoa Agizo kwa Wenza Waliotelekezana Kujisalimisha Polisi Kuanzia Sasa.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi ,Bw.Juma Homera.
Na Auleria Gabiel –RK Katavi.

Mkuu wa mkoa wa Katavi Bw. Juma Homera ametoa siku 14 kwa Wazazi waliotelekeza familia zao mkoani humo, kujisalimisha kwa jeshi la polisi,kabla hawajatafutwa.

Bw. Homera ametoa maagizo hayo Otober 28,2019, wakati akisikiliza kero za wananchi waliokusanyika katika ukumbi wa halmashauri ya manispaa ya Mpanda, ambapo wanawake 10 walijitokeza, wakilalamikia kutelekezwa na wenza wao.

Katika mkutano huo,Mzee mmoja akilalamikia kukimbiwa na mke wake baada ya kumuibia pesa za pensheni alizozipata.

Mkuu  huyo wa mkoa wa Katavi ,amesema hiyo ni hali isiyovumilika ndani ya mkoa  huo na kuwataka Wazazi wote wanaofanya tabia hiyo kuacha mara moja tabia hiyo.

Mkuu wa mkoa wa Katavi, Bw. Juma Homera ameweka utaratibu wa kusikiliza kero mbali mbali za wananchi kila ifikapo mwisho wa mwezi na kwa mwezi huu wa October wamejitokeza zaidi ya wananchi 200 kutoka maeneo mbalimbali ya wilaya za mkoa huo wakiwa na matatizo ya kifamilia, madai na mengineyo.

Post a Comment

0 Comments