habari Mpya


Rais Magufuli Kuhakiki Dola Milioni 14 Zilizokusanya na Shirika la Ndege la Tanzania.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akiwa katika kiti cha rubani  Boeing 787-8 Dreamliner alipoipokea
katika Uwanja  wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es
Salaam Jumamosi Oktoba 26, 2019.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akimpongeza Kepteni Saidi Hamadi mmoja wa Marubani walioleta ndege ya  Boeing 787-8 Dreamliner kuoka Seattle Marekani alipoipokea katika
Uwanja  wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam
Jumamosi Oktoba 26, 2019.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakifurahia jambo baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuipokea ndege mpya ya Boeing 787-8 Dreamliner.
Shirika la ndege Tanzania (ATCL) limekusanya Dola  milioni 14  tangu lilipoanza upya kufanya safari mbalimbali za ndege nchini.

Akizungumza wakati wa kupokea ndege mpya ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) aina ya Boeing Dreamliner 787-8 katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam , Rais  wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amesema Leo Oktoba 27 ataenda kuhakikisha fedha hizo.

Ndege hiyo kubwa yenye uwezo wa kuchukua abiria 262 , inakuwa ndege ya 7 kati ya ndege 11 zilizonunuliwa na Serikali kwa lengo la kuimarisha Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), kukuza utalii na uchumi.

Kwa mujibu wa Rais Magufuli amesema ndege hiyo mpya ya Boeing 787-8 Dreamliner ni ndege kubwa ya kisasa yenye uwezo wa kubeba abiria 262 ikiwemo abiria 22 wa daraja la juu pamoja abiria 240 katika daraja la kawaida, hivyo kuitaka ATCL kuweka mipango na mikakati endelevu ya kuhakikisha itangaza vyema vivutio vya utalii vilivyopo nchini.

Rais Dkt. John Magufuli amesema Tanzania itaendelea kutekeleza kwa kasi kubwa miradi ya maendeleo nchini kwa kuwa Serikali imeimarisha nidhamu katika usimamizi na matumizi ya rasilimali zilizopo pamoja na ukusanyaji wa kodi.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dkt. Leonard Chamuriho amesema Shirika la ATCL limeendelea kutekeleza kwa mafanikio makubwa Mpango Mkakati wa Shirika hilo, ambapo sasa limeweza kufikia mafanikio ya asilimia 73 la usafirishaji wa abiria katika soko la ndani.

Post a Comment

0 Comments