habari Mpya


Ngara –‘’Maiti Yakaa Siku Nne Mto Ruvubu Bila Kuopolewa’’.

Makutano ya Mto Kagera na Ruvubu wilayani Ngara,Kagera.

Picha / Habari Na Simon Dioniz –RK 97.9 Ngara.

Wakazi wa kijiji cha Rusumo wilayani Ngara mkoani Kagera wameilalamikia Serikali wilayani humo, kwa kushindwa kuondoa maiti  ya mtu anayeonekana katika eneo la mto Kagera ikielea kwa muda wa siku zaidi ya nne licha ya ripoti kutolewa kwa viongozi wa eneo hilo huku kukiwa hakuna jitihada zinazofanyika za kuondoa maiti hiyo.

Wakiongea na Radio Kwizera ,Wananchi hao wamesema kuwa maiti hiyo ilianza kuonekana tangu jumanne  lakini hadi leo ijumaa hakuna jitihada zinazoonekana kufanywa  ili kuiondoa maiti hiyo ambapo kwa sasa imeanza kuharibika  huku eneo hilo likitanda harufu  mbaya. 

BOFYA HAPA PLAY KUISIKILIZA RIPOTI YA MWANAHABARI WETU SIMON DIONIZ.

Post a Comment

0 Comments