habari Mpya


Watu 12 Wanaoshukiwa ni Majambazi Wauawa na Polisi Kibondo.

Muonekano wa risasi zilizokamatwa katika tukio hilo la September 12,2019.

Picha/Habari Na James Jovin –Kibondo.

Watu 12 wanaodhaniwa kuwa ni Majambazi wameuawa baada ya kupigwa risasi na Jeshi la Polisi wakati wakijaribu kufanya utekaji wa magari katika barabara kuu ya kuingia mjini Kibondo mkoani Kigoma.
Akizungumza akiwa katika eneo la tukio katika kijiji cha Kilemba wilayani humo, Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma Martin Otieno amesema tukio hilo limetokea Septemba 12,2019 majira ya saa tatu za usiku.
Aidha Kamanda Otieno amesema kuwa majambazi hao walikutwa na silaha ikiweom ya AK 47, risasi 107 zilizokuwa ndani ya Magazine sita, mabomu mawili ya kutupa kwa mkono pamoja na mapanga sita waliyokuwa wakitumia katika shughuli yao ya utekaji.
Kamanda Martin Otieno amesema kuwa mafanikio ya kuuwawa kwa watu hao yametokana na ushirikiano mzuri wa Jeshi la Polisi la Burundi mkoa wa Ruyigi baada ya kuwasiliana na kupeana taarifa zilizosaidia kuuwawa kwa watu hao.

Post a Comment

0 Comments