habari Mpya


Wafanyabiashara Walia na Miundombinu Mibovu ya Soko Ngara Mjini.

Wananchi na Wafanyabiashara wamekuwa wakikosoa kuhusu soko hilo halina hadhi kulingana na mahitaji ya Wananchi na mabadiliko ya hali ya hewa -Picha na Maktaba Yetu.

Wafanyabiashara wa soko kuu la Halmashauri ya Wilaya ya Ngara mkoani Kagera bado wanaililia serikali kuwaimarishia miundombinu ya soko, ili kuendana na hadhi ya masoko mengine kwani soko hilo halijafanyiwa marekebisho kwa kipindi kirefu.

Wakizungumza na Radio Kwizera sokoni hapo, baadhi ya wafanyabiashara wamesema soko la Ngara mjini linatumiwa pia na raia wa kigeni hivyo ni aibu kwa soko ambalo linategemewa na idadi kubwa ya watu, kutokuwa na vigezo.

Wamesema wanapata shida hasa msimu wa mvua unapoonza kwani biashara zao zinanyeshewa na kuharibika, nan i kwa muda mrefu wameomba kuboreshewa lakini bado hawajaona mabadiliko.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Mamlaka ya mji mdogo wa Ngara BW. JULIAS BUKOBERO amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo, na amesema halmashauri imeishafanya makisio ya bajeti ya kwanza kwa ajili ya ukarabati wa soko hilo, na tayari wanaendelea kufanya makisio ya bei ya vifaa kwa ajili ya kuanza ujenzi ndani ya mwaka wa fedha 2019/2020.

Post a Comment

0 Comments