habari Mpya


Wadau Jijini Mwanza Waelimishwa Kuhusu Ufungaji wa Umeme.

Zaidi ya Wadau 140 wa Nishati ya Umeme Kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa wamepatiwa Semina ya Kuwajengea uwezo  katika Shughuli za Ufungaji wa Umeme Jijini Mwanza.

Akizungumza  Wakati wa kuhitisha  Semina hiyo ya Siku tatu Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Ziwa Mhandisi George Mhina amewataka washiriki Hao Kufanya Kazi kwa Kuzingatia Sheria Za Nchi ikiwa ni Pamoja na Kujiepusha na Vitendo vya kuomba au kupokea Rushwa.
Kwa Upande wao Baadhi ya Washiriki wa Senina hiyo wamesema kuwa watakuwa mabalozi kwa wenzao na kuhakikisha wanafanya kazi kwa kuzingatia viwango , Sheria  na taratibu zilizowekwa na mamlaka.
Hata Hivyo kwa Upande wake Mhandisi Emmanuel Kachewa Meneja wa Tanesco Mkoa wa Mara na Mhandisi Masingija Jeremia Rugata Meneja wa Tanesco Mkoa wa Kigoma wamesema kuwa wanaimani na Mafuzo hayo waliopatiwa Mafundi umeme na itasaidi kuondokana na changamoto mbalimbali zilizokuwa hapo awali.

Post a Comment

0 Comments