habari Mpya


Serikali Yaitaka Hospitali ya Nyamiaga wilayani Ngara Kutumia Bajeti za Ndani Kununua Mashine za Kufulia Nguo.

Bungeni Dodoma.

Mganga Mkuu Mfawidhi wa hospitali ya Nyamiaga kwa kushirikiana na Mganga Mkuu wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera wametakiwa kutumia Bajeti za ndani ili kuhakikisha wananunua mashine za kufulia Nguo katika hospitali hiyo.

 Agizo hilo limetolewa September 13,2019 na Naibu Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto Dr. Faustine Ndugulile wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu mkoani Kagera Bi.Oliva Semuguruka ambaye alitaka kufahamu mpango wa Serikali katika kununua Mashine za kufulia Nguo katika Hospitali hiyo.

Akitoa majibu, Naibu Waziri Ndugulile amesema mashine za kufulia hazina gharama kubwa hivyo wafanye jitihana kununua.

SIKILIZA HAPA CHINI MASWALI NA MAJIBU HAYA BUNGENI.
Kadhalika Dr. Ndugulile ameongeza kuwa, vituo vya kutolea huduma za afya hufanya makusanyo ya fedha na Serikali hutoa fedha hivyo vinapaswa kujiendesha kwa vitu ambavyo havina gharama kubwa.

Post a Comment

0 Comments