habari Mpya


Redio Kwizera ya Ngara Yatajwa Kuleta Mabadiliko Sekta ya Kilimo Nchini.

Na Anord Kailembo –RK Bukoba 97.7.


Redio Kwizera ya Wilayani Ngara mkoani Kagera imetajwa kuwa na mchango mkubwa katika mabadiliko yanaoonekana kwenye Sekta ya Kilimo ambapo kwa sasa Wakulima wanaondokana na kilimo cha mazoea na kwenda kwenye kilimo biashara hasa kwenye maeneo unakotekelezwa mradi wa TIJA Tanzania.

Hayo yameelezwa na BW. FRANK ADEMBA Afisa Mradi wa TIJA TANZANIA wakati akizungumza na redio kwizera na kwamba kwa utafiti uliofanywa na Shirika hilo wamebaini kupitia KIPINDI CHA KILIMO BORA kinachorushwa Redio Kwizera kimekuwa mwongozo kwa Mkulima kujua ni namna gani anaweza kulima kwa tija.

Aidha amesema kuwa kipindi hicho kimewasaidia kuzifahamu changamoto mbalimbali zinazowakabili wakulima na kwamba mradi huo utaendelea kushirikiana na REDIO KWIZERA katika kuhakikisha wanawasaidia Wakulima kupiga hatua kupitia kilimo.

Kwa upande wao baadhi ya wadau wa kilimo wamesema kuwa Redio za Kijamii zimekuwa msaada mkubwa kwa Wakulima kwani asilimia kubwa ya wakulima husikiliza vyombo hivyo ili kufahamu mambo mbalimbali yanayowagusa ikiwemo shughuli za kilimo na kushauri ziendelee kutumika kuwaelimisha Wakulima.

Post a Comment

0 Comments