habari Mpya


NELSAP Haitatoa Fidia Kwa Wananchi Ngara Mradi wa Maji Utakapopita.

Maji ya Mto Ruvuvu katika eneo la Rusumo,Ngara mkoani Kagera.
Shirika la NELSAP linalosimamia miradi mbali mbali wilayani Ngara Mkoani Kagera inayofadhiliwa na benki ya dunia limesema hawatakuwa na fidia kwa wananchi wenye mashamba litakapopita bomba la maji yatakayotoka kwenye mto ruvuvu uliopo wilayani humo.

Mratibu wa  usimamizi wa miradi hiyo  kutoka shirika hilo kwa nchi za Rwanda, Tanzania na Burundi Bw. Hamdun Mansur amesema  shirika lina fedha  kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa maji pekee katika vijiji vyote vya kata za Rusumo na Kasulo  hivyo halmashauri inatakiwa kuwaelewesha wananchi wake mapema.

Amesema kuna tabia ya baadhi ya wananchi pindi miradi mikubwa inapotekelezwa huomba fidia hasa pale inapopita na kwamba kwa sasa ni kuhakikisha wananchi wanaupokea mradi na kuukubali ili utekelezaji uendelee.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Rusumo Bw. Dauson Kadende amesema tayari Wananchi wamehamasishwa kuhusu suala hilo na wamekubaliana kuhusu mradi huo hivyo hakutakua na tatizo lolote katika utekelezaji.

Post a Comment

0 Comments