habari Mpya


Magunia 392 ya Kahawa ya Magendo Yakamatwa Ngara.

Magunia ya Kahawa ya Magendo yaliyowahikukamatwa Mkoani Kagrea-Picha na Maktaba Yetu.

Halmashauri ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera imekamata magunia 392 ya Kahawa ya Magendo kutoka vijiji vya Kanazi, Mrutabo na Mwivuza kuanzia mwanzoni mwa Mwezi huu wa September, 2019.


Akizungumza na watendaji wa kata wilayani Ngara, Mkuuu wa wilaya ya Ngara Luteni Kanali Michael Mtenjele amewataja waliokamatwa na Kahawa hizo za magendo kuwa ni Charles James Korongo, Peter Boaz John, David Dastan, Abmerick Elisha, Zakayo Mika, Haruna Juma John, Gwassa Emmanuel na Fikiri Brighton ambao wote kahawa yao itataifishwa na watafikishwa mahakamani.

Luteni Kanali Mtenjele amesema msako huo ulihusisha Maafisabiashara, Maafisa kutoka Usalama wa Taifa na Jeshi la Polisi ambapo wamefanikiwa kukamatwa kwa wafanyabiashara hao ambao wameanza ununuzi wa Kahawa kutoka kwa Wakulima kinyume cha sheria na taratibu.

Kufuatia tukio hilo, amewataka Watendaji wote wa Ngara,kuendelea kutoa taarifa kwa Mamlaka juu ya Wafanyabiashara na Wakulima ambao wanaendelea na tabia ya kuuza Kahawa ya magendo kinyume na sheria zinazotakiwa. 

Post a Comment

0 Comments