habari Mpya


Maeneo ya MUGOMA, RUGANZO na KIRUSHYA Vinara wa Kuuza Kahawa Mbichi Wilayani Ngara.

Na Simon Dioniz -RK Ngara 97.9 Mhz.

Chama cha Wakulima Ngara Farmers Wilayani Ngara Mkoani Kagera huenda kikapata hasara badaa ya Mawakala waliowatuma kununua kahawa kuinunua ikiwa bando mbichi zaidi ya tani 60 yenye thamani ya shilingi milioni 50.

Maeneo ambayo yamebainika kununua kahawa mbichi ni pamoja na MUGOMA, RUGANZO na KIRUSHYA ambapo  baada ya kuipima imekutwa ikiwa na unyevu wa kiwango cha   asilimia 14.7 ambacho ni kikubwa kinachoweza kuharibu kahawa yote.
Akizungumza na Radio Kwizera, Mwenyekiti wa Chama hicho wilayani Ngara BW. DAVID BUKOZO amesema kutokana na dosari za ununuzi zilizojitokeza wamelazimika kusitisha ununuzi wa kahawa hadi Oktoba 01 mwaka huu,2019.

BW.BUKOZO  amewataka Wakulima kuhakikisha wanaanika upya kahawa ili watakapoanza tena ununuzi wa kahawa iwe imekauka na kwamba hawatanunua kahawa endapo itakuwa mbichi ili kuepuka hasara.

ZAIDI BOFYA PLAY HAPA CHINI KUSIKILIZA.

Post a Comment

0 Comments