habari Mpya


Lori la Gesi Lapata Ajali na Kuua Dereva na Mpanda Baiskeli -Rusumo Ngara.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo ,Kaimu Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wilaya ya Ngara mkoani Kagera, Denis  Minja  amesema tukio hilo limetokea  leo September 9,2019 majira ya saa tisa alasiri katika eneo la Boda ya Rusumo ambapo Lori aina ya FAW lenye namba za usajili T 484 DPX    kampuni ya CAMEL ambalo lilikuwa limebeba Gas liliferi mfumo wa breki na kuanguka wakati likitokea Dar Es Salam kuelekea nchini Rwanda.

Aidha ulinzi umeimarishwa kulinda Gesi inayovuja isilete madhara kwa Wananchi.
Katika ajali hiyo waliofariki ni Dereva wa Lori kwa kubana na kebin Jina Evans John Alfonsi mkazi wa Dar Es Salaam ambaye alifariki papo hapo.

Aliyefariki mwingine ni mpanda baiskeli akitoka kununua bidhaa Tanzania ,akielekea Rwanda na ajali hiyo kumkuta eneo la getini akitaka kuvuka mpaka anajulikana kwa jina la Abumugisha Thomas.
 

Post a Comment

0 Comments