habari Mpya


Story 7 Yaliyojiri Kahama,Biharamulo,Geita,Buhigwe,Kasulu,Ngara na Kakonko.

Askofu Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amebariki jumla ya mawe saba ya msingi kwa ajili ya kuanza ujenzi wa nyumba za Mapadri,Watawa na Shule za Secondari wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Mwanahabari wetu Faraja Marko anataarifa Zaidi Kutoka Kahama- FARAJA


Wananchi  wa wilaya ya Nyang’hwale Mkoani Geita  wamelalamikia umbali wa vituo vya afya na zahahati, hali inayowalazimu  kutembea umbali wa zaidi ya kilomita 10 wakifuata huduma za afya licha ya kuwepo majengo mapya ya zahanati ambayo hayajaanza kutumika.


Taarifa ya Mwanahabari wetu Gibson Mika Inafafanua kutoka Wilayani Nyang'hwale Mkoani Geita- GIBSON


Zaidi ya asilimia 50 ya wananwake katika wilaya ya Buhigwe , imetajwa kutokuwa na uelewa wa kutosha kuhusu  taratibu za unyonyeshaji , kutokana na mitazamo potofu juu namna ya unyonyeshaji watoto hadi umri wa miaka miwili.


Mwanahabari wetu Philmon Golkanus anataarifa Zaidi kutoka Wilayani Buhigwe Mkoani Kigoma- GOLKANUS


Halmashauri wilaya ya Ngara Mkoani Kagera imekili kuwa na upungufu mkubwa wa vyumba vya maabara katika shule za sekondari licha ya serikali kutoa fedha nyingi kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya Sayansi  katika shule hizo jambo ambalo limechangia vifaa hivyo kuhifadhiwa kwenye vyumba vya madarasa.


Mwanahabari wetu Simon Dioniz Amefanya mazungumzo na Afisa Elimu Shule za Sekondari Bw. Enock Ntagisigaye akitaka kujua  hali halisi ya ufundishaji wa somo la Sayansi kwenye shule hizo- DIONIZ  


Halmashauri ya Mji wa Kasulu Mkoani Kigoma imesonga Mbele  kwa kudhibiti ukosefu wa vyoo katika jamii na kufikia kiwango cha Asilimia 2 ya kaya  zisizo na vyoo ndani ya mji huo huku wasio na vyoo wakichukuliwa hatua za kisheria.


Taarifa ya Mwanahabari wetu Albert Kavano inafafanua Zaidi kutoka Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma- KAVANO


Mahakama  ya wilaya ya Biharamulo  mkoani Kagera  imewahukumu watu 4 wakazi wa Kitwechembogo kata ya Ruziba  wilaya ya Biharamulo kutumikia  kifungo  cha miaka 20 gerezani  kila mmoja   au kulipa  faini ya shilingi milioni  42  baada ya kupatiakana  na hatia  ya makosa matano.


 Mwanahabari wetu William Mpanju anataarifa Zaidi kutoka Wilayani biharamulo Mkoani Kagera- MPANJU


Baadhi ya wananchi wilayani Kakonko Mkoani Kigoma  wameuomba uongozi wa halimashauri hiyo kuendelea kusimamia mashirika na makampuni ya nayo omba kazi wilayani humo kutoa ajira kwa wazawa kuliko kuajiri wageni kutoka nje ya wilaya husika  ili wananchi waweze kunufaika na kuinua uchumi wa familia zao.


Kutoka Wilayani Kakonko Mkoani Kigoma Mwanahabari wetu Amos John anataarifa Zaidi-AMOS

Post a Comment

0 Comments