habari Mpya


Askofu Niwemugizi:Walimu wa andaeni wanafunzi kujibu vizuri Mitihani yao

Picha na Godfrey Bisambi/Habari na Simon Dionizi
Mhasham Baba Askofu wa Kanisaa katoliki jimbo katoliki la Rulenge Ngara Askofu Severine Niwemugizi amewaagiza wakuu wa shule zinazomilikiwa na kanisa hilo kuhakikisha wanafundisha kwa kufuata maadili na maelekezo ya serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania


Kauli hiyo ameitoa wakati akizindua shule ya msingi inayofundisha kwa Lugha ya Kiingereza inayomilikiwa na shirika la Masista la wafransisiko wa Mt. Bernadetha iliyopo kijiji cha Mumitelama wilayani Ngara Mkoani Kagera ambayo inajulikana kwajina la Mt. Boneventure

Amesema hataki kusikia taarifa au kuona moja ya shule zinazomilikiwa na Kanisa Katoliki zikijihusisha na vitendo vya uvujishaji wa Mtihani na kwamba mwanafunzi atakayetegemea kubebwa anatakiwa kusahau na kuhakikisha anajitegemea

Amesema kuwa kila mwalimu wa shule hiyo anatakiwa kuhakikisha anafundisha kwa lengo la kumusaidia mwanafunzi kufanya vizuri katika mtihani na sio mwanafunzi ategemee kufanyiwa mtihani na kwamba mwanafunzi anayo toka katika shule hizo awe mfano wa kuigwa ndani na nje ya nchi.


Post a Comment

0 Comments