habari Mpya


Afisa Mtendaji wa Kijiji Atoroka na 285,000 Za Wananchi Biharamulo.

Baadhi ya  Wananchi  wa kijiji  cha Songambele kata ya Nyamigogo  Wilayani Biharamulo mkoani  Kagera wameshindwa  kukamilisha  ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho baada ya aliye kuwa afisa mtendaji wa kijiji hicho  Thobias  Kapesa kutoroka na   fedha za michango ya wananchi.

Wakiongea na radio Kwizera kwa nyakati tofauti wamesema  zahanati yao  imeshindwa  kukamilika  zaidi ya  miezi miwili kufuatia fedha  ambazo ni michango yao kutoroshwa na aliyekuwa mtendaji wa kijiji hicho.

Wamesema baada ya mtendaji kutoroka na fedha za wananchi zaidi ya shilingi laki mbili wameshindwa kuendelea kuchangia fedha za ujenzi wa zahanati kutokana na kukosa mtendaji wa kukusanya michango na kuwasomea mapato na matumizi.

SIKILIZA ZAIDI SAKATA HILI HAPA.

Post a Comment

0 Comments