habari Mpya


Waumini wa Kikatoliki Ngara Wamkumbuka Mwanzilishi wa Jimbo Katoliki la Rulenge Askofu Alfred Lanctot.

Hayati  Mhashamu Askofu Alfred Lanctot.

Waumini wa Jimbo katoliki la Rulenge Ngara mkoani Kagera May 30,2019 waadhimisha  miaka 50 ya kifo cha  Mwanzilishi wa Jimbo Katoliki la Rulenge  Mhashamu Askofu Alfred Lanctot aliyefariki  May 30,1969.

 Marehemu Askofu Alfred enzi cha uhai wake wakati akifanya UTUME wake katika Jimbo Katoliki la Rulenge wakati huo kabla halijawa Jimbo la Rulenge Ngara alifanya mambo mengi ikiwemo KUANZISHA  SHIRIKA LA WABERNADETHA LA MT.FRANSISCO WA ASIZI.

Amina Semagogwa (Msikilize hapa chini) amezungumza na  Askofu wa Jimbo Katoliki la Rulenge Ngara Severyne Niwemugizi na ameanza kwa kumuuliza ni kwa namna  gani ameweza kuzitimiza ndoto alizokuwa nazo Askofu Alfred Lanctot katika kulijenga na kuliendeleza Jimbo Katoliki la Rulenge Ngara.

AMINA SEMAGOGWA


HAPA CHINI SIKILIZA WASIFU WA MAREHEMU ASKOFU ALFRED LANCTOT.

AULERIA GABRIEL

Post a Comment

0 Comments