habari Mpya


Uhaba wa Vyuo vya Madrasa Muleba Chanzo cha Utovu wa Nidhamu kwa Watoto.

Kutokuwepo kwa mishahara ya uhakika kwa Walimu wa kufundisha elimu ya dini ya kiislamu pamoja na uhaba wa vyuo vya madrasa kwa baadhi ya misikiti wilayani Muleba mkoani Kagera, imetajwa kuwa Chanzo cha ongezeko la utovu wa nidhamu kwa baadhi ya watoto kutokana na kuwa na elimu duni ya dini hiyo.

Akizungumza kwenye Baraza  la Eid el Fitr lililofanyika ki wilaya katika msikiti wa AL NURU uliopo kata ya Kishanda, mwakilishi wa Imamu wa msikiti huo Rajabu Rozo amesema msikiti huo una waumini zaidi ya 500 lakini hakuna chuo cha madrasa.

Rozo amesema hali hiyo inakwamisha maendeleo ya msikiti pamoja na waumini, hivyo ameomba Baraza kuu la Waislamu Wilayani humo BAKWATA kuhakikisha linatoa kipaumbele kwa Walimu hao na wanapata stahiki zao kwa wakati pamoja na kujenga vyuo vya madrasa.
Naye Mwenyekiti wa Baraza kuu la Waislamu Wilayani Muleba Bakwata Shekh Husein Rugaimukamu ambaye alikuwa mgeni rasmi katika baraza hilo la Eid,amesema wamekuwa wakitembelea kila msikiti ambao hauna vyuo vya madrasa kuhakikisha wanahamasisha waumini wanajenga vyuo vya madrasa hasa maeneo ya vijijini.

Post a Comment

0 Comments