habari Mpya


Tanzania Yatarajia Kuzalisha Kilo milioni 400 za Pamba Msimu huu.

Pamba ikiwa Shambani.
Wakulima wa zao la Pamba nchini wametakiwa kuacha kulima kwa mazoea na badala yake kulima kwa kufuata teknolojia za kisasa ili kuweza kunufaika na zao hilo.
Akizungumaza katika shamba la mfano katika kijiji cha Nguge kilichopo wilayani Misungwi mkoani Mwanza Mtafiti wa zao la Pamba kutoka taasisi ya utafiti Ukiriguru Dkt. Furaha Mroso amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha kila mkulima wa zao la pamba nchini analima kwa tija ili kuongeza kipato.
MSIKILIZE HAPA Dkt.FURAHA MROSO.
Wakizungumza na Radio Kwizera katika shamba hilo la mfano, wakulima ambao wamepatiwa elimu ya kulima kwa kutumia teknolojia ya kupanda mbegu kwa kutumia mistari, wamesema tangu wameanza kupatiwa elimu hiyo wamenufaika kwa kupata mavuno mengi.
HAPA WAKULIMA WA ZAO PAMBA
Zao la Pamba ni moja kati ya mazao manane ya kimkakati nchini Tanzania ambapo msimu huu taifa linatarajia kuzalisha kilo milioni 400 za Pamba.

Post a Comment

0 Comments