habari Mpya


Taifa Stars Na Bendera ya Taifa yenye Matumaini tele AFCON 2019.

Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza akimkabidhi bendera Nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta tayari kwa safari ambapo kikosi cha timu ya Taifa kitaondoka kesho June 7,2019  kwenda nchini Misri kuweka kambi ya wiki mbili kikijiandaa na AFCON. 
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Juliana Shonza amesisitiza nidhamu kwa wachezaji timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kuelekea fainali za Mataifa ya Afrika 'Afcon'.

Shonza ameiaga Stars iliyowekwa kambini hoteli ya Whitesands inatarajiwa kusafiri kesho kwenda Misri wataendelea na kambi ya wiki mbili kabla ya kuanza kwa fainali hizo za Afcon.

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji, nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta amesema anaishukuru Serikali kwa kuwaunga mkono na watajituma ili kufanya vizuri katika fainali hizo.

Taifa Stars itaondoka na wachezaji 32 kwenda kambini mjini Alexandria, Misri baada ya kuchujwa saba na kati ya hao ni 23 tu watashiriki AFCON.

Wachezaji wengine wataendelea kubaki kambini kwa maandalizi ya michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN), inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee.

Kikosi cha kocha Mnigeria, Emmanuel Amunike kitaanza na mchezo wa kirafiki dhidi ya wenyeji wa AFCON, Misri Juni 13, mwaka huu Uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandria.

Baada ya hapo Taifa Stars itacheza mechi zake tatu za Kundi C mfululizo ikianza na Senegal Juni 23, Kenya Juni 27 na kumaliza na Algeria Julai 1 kuangalia matokeo yake kama yataipeleka hatua ya mtoano.

Post a Comment

0 Comments