habari Mpya


Rais Dkt. John Magufuli Awataka Viongozi Ngazi zote Kufanya Kazi kwa Kujituma ili Kuwafikishia Wananchi Maendeleo ya Kweli.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akimuapisha Bw. Innocent Lugha Bashungwa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara , Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 10, 2019.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Bw. Edwin Mhede kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Ikulu jijini Dar es salaam Jumatatu Juni 10, 2019.
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amewataka viongozi katika ngazi zote kufanya kazi kwa kujituma na kwa ushirikiano ili kuwafikishia wananchi maendeleo ya kweli.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo jioni ya leo June 10, 2019 ikulu jijini Dar es salaam, mara baada ya kuwaapisha viongozi aliowateua mwishoni mwa wiki iliyopita.

Amesema serikali ya awamu ya tano iliahidi kuwapatia maendeleo wananchi hivyo ni vema kila kiongozi kuwajibika ipasavyo akiwa madarakani kwani hakuna mwenye ajira ya milele.

MSIKILIZE HAPA RAIS MAGUFULI.

Viongozi walioapishwa na rais ni pamoja na Innocent Bashungwa ambaye sasa ni waziri wa Viwanda na Biashara akichukua nafasi ya Joseph Kakunda.

Wengine ni Edwin Mhede ambaye amekuwa Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), akichukua nafasi ya Charles Kichere ambaye kwa sasa ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe akichukua nafasi ya Erick Shitindi ambaye amestaafu.

Pia, Rais Magufuli amepokea gawio la Tsh bilioni 3 kutoka kampuni ya mawasiliano ya Bhart Airtel ambayo inamilikiwa  na serikali kama mwanahisa na Tsh bilioni 2.57, ambayo wamekabidhi ikulu kama pongezi kutokana na mambo makubwa yanayofanywa na serikali.

Post a Comment

0 Comments