habari Mpya


Uchomaji Taka Eneo la Makazi,Kero kwa Wananchi hawa Biharamulo.

Na Wiliam Mpanju – RK Biharamulo. 

Baadhi ya wakazi na Wafanyabiashara   wa soko la zamani  Kasusula  maarufu soko la  Wakuilma   mjini  Biharamulo, wilaya ya  Biharamulo  mkoani  Kagera  wamelalamia hatua ya idara ya Mazingira wilayani humo, kuanza kuchoma taka kwenye   dampo la jirani na soko hilo  badala ya kuziondoa  na kuzipeleka  eneo la kuhifadhia taka nje ya mji huo hali iliyosababisha  moshi wa taka hizo kuwa kero kwa wananchi.


Mara  kadhaa  taka hizo  zimekuwa  zikipigiwa kelele  na Wananchi kwa kusababisha harufu  mbaya  kutokana na madampo hayo  kuwa karibu na  maeneo ya makazi, mighahawa na maeneo wanakouzia  bidhaa za vyakula   lakini  bado  halmashauri  imeshindwa kutekeleza  hata agizo  alilolitoa  mkuu wa wilaya hiyo Bi Sada  Malunde  baada ya Wananchi kulalamika.

Kufuatia  kushindwa  kuzolewa kwa taka  hizo  maafisa  mazingira  wanatuhumiwa  kuchoma  taka hizo  ambazo  moshi wake  unadaiwa kuwa  chanzo cha uchafuzi wa mazingira na kudaiwa kuwa   kero  kwa wafanyabiashara  wa soko hilo  na mamalishe    ambapo Radio kwizera  imeshuhudia  moshi mkubwa ukifuka eneo hilo  na kusambaa maeneo  mbalimbali ya mjini huo na afisa mazingira alipotafutwa  hakuweza kupatikana na simu yake iliita bila kupokelewa.

Post a Comment

0 Comments