habari Mpya


Mwanafunzi wa Darasa la Saba Biharamulo Aacha Masomo kwa Ujauzito.

Na Wiliam Mpanju – RK Biharamulo. 

Mwanafunzi wa  darasa la saba shule ya msingi  Kisuno kata ya Bisibo wilayani  Biharamulo  mkoani  Kagera amesimamishwa  masomo baada ya kubainika  kuwa na ujauzito.

 Mwalimu mkuu wa shule hiyo Bw. Charles  Marco  amesema mwanafunzi  huyo  mwenye umri wa miaka 17 amebainika  baada ya uchunguzi  kutoka kwa wataalam wa afya na wazazi  na kubaini kuwa na ujauzito wa miezi 4.

 Amesema  Mwanafunzi huyo  amekatishwa ndoto zake  na kwamba   alitarajia  kuungana na wenzake  mwezi September mwaka huu,2019  kufanya mtihani wa kitaifa wa kuhitimu darasa la saba na huenda  angechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza.

 Naye Afisa Mtendaji wa kijiji hicho  Bw. Venas Rukamata  amesema  baada ya kupewa taarifa hizo na Mwalimu Mkuu  wanaendelea  kufuatilia  kijana  anayetuhumiwa  kumsababishia ujauzito  ambaye hakutaka jina lake litajwe ili kutoharibu upelekezi ili hatua ziweze kuchukuliwa dhidi yake.

Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi  wilayani Biharamulo  Bw. Mudhuwari  Msuya  amesema  wanaendelea kumtafuta  mtuhumiwa  anayedaiwa  kufanya kitendo hicho  ili wamfikishe  kwenye  vyombo  vya sheria.

Post a Comment

0 Comments