habari Mpya


Mama Amchinja Mtoto wake na Kumpika Kama Supu.

Na Gibson Mika –RK GEITA 90.5

Mwanamke mmoja miaka 36, mkazi wa kijiji cha Burigi Kata ya Senga mkoani Geita anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani humo kwa tuhuma za kumchinja mwanae na kisha kumpika.

 Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kwa njia ya simu Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani humo, Dismas Kisusi amesema tukio hilo limetokea june 21 mwaka huu  saa nane Mchana kijijini humo na kwamba mama huyo alimkatakata mwanae vipande vidogo vidogo kisa kuviweka ndani ya sufuria na kuvichemsha.

Amemtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Happyness Shadrack ambaye anadaia kuwa na tatizo la akili na kwamba Jeshi hilo linaendelea na uchunguzi wa kina juu ya tukio hilo.

SIKILIZA HAPA.


Aidha mwenyekiti wa serikali ya Kijiji cha Buligi Farigi Mwarabu amesema mama huyo alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya akili kwa muda mrefu kabla ya kutekeleza tukio hilo nahivyo kuiomba serikali kuchunguza kwa kina juu ya tukio hilo.

Post a Comment

0 Comments