habari Mpya


Jeshi la Polisi mkoani Kigoma latoa tahadhari kwa wananchi wanao piga simu kutoa taarifa za uongo za matukio ya Moto

KIGOMA: Na, Adrian Eustace
Jeshi la zima moto na uokoaji mkoa wa Kigoma limetoa tahadhari kwa wananchi wanaopiga simu na kutoa taarifa za uongo juu ya uwepo wa matukio ya moto katika maeneo yao


Akizungumza na Redio Kwizera ofisini kwake, kaimu kamanda wa jeshi la zima moto na uokoaji mkoa wa Kigoma mkaguzi msaidizi Malumbo Ngata amesema baadhi ya wananchi wasio waadilifu wanapiga simu kupitia namba ya bure ya jeshi hilo kutoa taarifa za uongo kuhusu matukio ya moto jambo ambalo ni kosa kisheria

Kadhalika Bw. Ngata amesema waumini Elfu Moja na 83 wa dini za Kikristu na Kiislamu mkoani Kigoma wamepatiwa elimu ya Kinga na Tahadhari ya moto iliyotolewa na Jeshi la Zima Moto na Uokoaji mkoani humo ikiwa ni hatua za kukabiliana na majanga ya moto pindi yanapojitokeza

Kwa upande wao baadhi ya wananchi mkoani Kigoma wameliomba jeshi la zima moto na uokoaji kuanzisha mfumo wa kuwabaini watu wanaotoa taarifa za uongo juu ya majanga ya moto na kwamba pindi wanapobainika wachukuliwe hatua za kisheria ili kuwa fundisho kwa watu wengine

Post a Comment

0 Comments