habari Mpya


Gashaza Ataka Vijana wa Vyuo Vikuu Wanaojitolea Kufundisha Ngara Waungwe mkono na Serikali.

Mbunge wa Jimbo la Ngara Bw.Alex Raphael Gashaza.


Serikali nchini imemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara na Afisa Elimu Sekondari kukutana na umoja wa vijana wa vyuo vikuu nchini wanaotoka wilayani Ngara mkoani Kagera ambao wamekuwa wakijitolea kufundisha katika shule za sikondari ili kuwawezesha. 

Kauli hiyo imetolewa Bungeni Jana June 10, 2019 jijini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe.Mwita Waitara wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Ngara Bw.Alex Raphael Gashaza.

Katika swali lake la Nyongeza, Mbunge Gashaza amehoji Vijana wanao soma vyuo vikuu nchi nzima wanaotoka wilayani Ngara kwa miaka miwili mfululizo wakati wa likizo ndefu wamekuwa wakijitolewa kufundisha katika shule za sekondari, je serikali haioni sababu ya kuwaunga mkono katika kazi hiyo.

…….GASHAZA.

Katika majibu yake Naibu Waziri wa TAMISEMI Mhe.Mwita Waitara amesema kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara na Afisa Elimu Sekondari wanapaswa kufanya mazungumzo na vijana hao kujua nini wanahitaji ili serikali iwaunge mkono.

…….WAITARA.

Post a Comment

0 Comments