habari Mpya


Waziri Lugola Asimamisha Kazi Wakuu wa Polisi Watatu Geita.


Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi KANGI LUGOLA amemuagiza Katibu wa Wizara ya Mambo ya ndani kuwasima Kazi Mkuu wa Polisi Wilaya ya Geita (OCD), Mkuu wa Kituo cha Polisi Geita(OCS) na Kaimu Mkuu wa Upelelezi Wilaya hiyo (OC CID),kwa kosa la Mahabusu kutoroka Mahakamani. 


Pia ameelekeza Askari 8 wa kituo hicho wawekwe Selo ili kupisha uchunguzi.


Agizo hilo amelitoa May 24, 2019 akiwa Mkoani Geita kufanya ufuatiliaji wa watu hao waliotoroka Mkoani Geita wakituhumiwa kwa makosa mbalimbali na kumtaka Mkuu wa mkoa kuhakikisha wanafanya uchunguzi na kuwakamata askari wote waliokuwepo doria.

WAZIRI LUGOLA

Nae Mkuu wa mkoa wa Geita amewataka wananchi wa mkoa huo wanapowabaini watu hao watoe taarifa kwenye vyombo vya sheria ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao.

MHANDISI GABRIEL

Haya yanajiri baada ya mahabusu waliokua wameshikiliwa katika kituo cha polisi cha Wilaya ya Geita kutoroka ambapo idadi yao ni 15 na wanne kati yao tayari wamekwishakamatwa.


Post a Comment

0 Comments