habari Mpya


Waziri AWESO 'Alivyomsweka' Ndani Mkandarasi Geita.

Na GIBSON MIKA –RK Geita 90.5.

Naibu Waziri wa Maji Nchini Juma Aweso akitoa maaagizo kukamatwa kwa Mkandarasi anayetekeleza mradi wa maji wa Nyamtukuza wilayani Nyang’hwale Mkoani Geita kwa kushindwa kutekeleza mradi huo kwa wakati hali inayopelekea  wananchi waliozunguka mradi huo kukosa huduma ya maji safi na salama.

 Naibu Waziri Aweso ametoa maagizo hayo hivi karibuni baada ya kutembelea mradi huo unaotekelezwa kwa  kiasi cha shilingi billion 15 na million 11 huku  Serikali ikiwa imeshamlipa  Mkandarasi huyo Mwaipopo Lukas  kutoka   Kampuni ya PET COPARATION  kiasi cha shilingi billion 8.
Juma Aweso.

Akizungumza na Wananchi katika Mkutano wa Hadhara,Naibu Waziri Aweso amesema mradi huo umeanza kutekelezwa mwaka 2014 na kwamba hadi sasa wananchi waliozunguka mradi huo  hawana uhakika wa kupata hata ndoo moja ya maji hali inayowalazimu kuendelea kutumia maji machafu.

Nao Wananchi wa kijiji cha Nyamtukuza wilayani humo, wamemuambia Waziri kuwa, tatizo la maji limekuwa shida kubwa kwao kutokana na kutumia maji ya kisima cha Ihelele ambacho pia wafugaji hutumia kunyweshea mifugo yao  hali inayosababisha wananchi kuugua magonjwa ya tumbo.

Katika hatua nyingine Mbunge wa Jimbo hilo Bw. Hussein Kasu ameiomba Serikali kuwapatia usafiri Wahandisi wa maji katika halmashauri  hiyo ili kuwa na usafiri wa uhakika utakaowasaidia  kufuatilia miradi ya maji inayotekelezwa kwa kina.

Post a Comment

0 Comments