habari Mpya


Picha 7:Basi la Arusha Express Lilivyotekea kwa Moto Bukoba.

Muonekano wa Basi la Kampuni ya Arusha Express lililokuwa likitoa huduma za usafiri wa abiria kati ya Bukoba mkoaki Kagera na Arusha likiwa limeteketea kwa moto alfajiri ya Jana May 21,2019 katika eneo la Kibeta, Manispaa ya Bukoba. 

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kagera Revocatus Malimi amesema kuwa gari hilo ni lenye namba za usajili T 222 ABF  na kwamba tukio hilo imetokea majira ya saa 12 asubuhi huku kukiwa hakuna abiria aliyejeruhiwa wala kuunguliwa na mizigo yao.
 
Kamanda Malimi amesema kuwa hakuna madhara yoyote  yaliyoripotiwa  kutokea wala chanzo cha moto huo hakijajulikana.
 
 
Aidha Kamanda Malimi amesema kuwa jeshi la polisi kupitia kitengo cha usalama barabarani kinapaswa kuhakikisha magari yote yanayosafirisha abiria na binafsi yanakaguliwa na kuzingatia usalama barabarani wakati zikiwa barabarani. 
 

Post a Comment

0 Comments