habari Mpya


Magonjwa yasiyo ya Kuambukiza Sababu ya Upungufu Watumishi wa Afya Nchini.

Kuongezeka kwa Magonjwa yasiyo ya kuambukiza kumetajwa kuwa moja ya sababu inasababisha upungufu wa wawatumishi wa sekta ya afya katika vituo mbalimbali vya afya hapa nchini ambapo kuna pengo la  asilimia 52 ya watumishi kote mchini.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. UMMY MWALIMU Jijini Dodoma, katika ufunguzi wa kikao cha kujadili changamoto za rasilimali watu katika sekta ya afya kati ya viongozi kutoka Wizara ya Afya, TAMISEMI na Washirika wa Maendeleo ya nchi.

Amesema wamekutana katika kikao hicho ili kujadili changamoto mbalimbali zinazohusu rasilimali watu ikiwemo ya upungufu wa watumishi, ajira, mafunzo pamoja na mahitaji ya watumishi kunzia ngazi za zahanati hadi hospitali za wilaya nchini.

 - UMMY MWALIMU

Aidha Waziri Ummy amesema  watajadili mikakati ya pamoja ya ubunifu kuona  kunakuwa na maboresho ya uzalishaji wa wataalam wa afya na wale wale wanaozalishwa ili kuona ni kiasi gani wanaweza kuajiriwa na kuwa watumishi wa umma hususan katika ngazi za zahanati na hospitali za wilaya nchini.

Post a Comment

0 Comments