
Jeshi
la Polisi nchini kupitia kitengo cha Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano (TEHAMA) kwa kushirikiana na Government e-Payment Gateway
(GePG) limeanzisha mfumo wa upatikanaji wa fomu ya upotevu (Police Loss
Report) kupitia mtandao wa https://Lormis.tpf.go.tz na kufanya malipo
kwa njia ya simu kwa mfumo wa GePG.
Mfumo huo ulianzishwa mwezi
Machi, 2019 na kitengo cha TEHAMA Makao Makuu ya Polisi kwa lengo la
kupunguza gharama na kurahisisha upatikanaji wake katika vituo vya
Polisi humuwezesha mtu yeyote kufanya maombi na malipo ya Loss Report
kwa njia ya mtandao na baadaye mwombaji kwenda Kituo cha Polisi ili
kukamilisha huduma hiyo.
Mwombaji wa fomu ya upotevu kwa njia ya mtandao, atatakiwa kufuata hatua zifuatazo:-
Mwombaji wa fomu ya upotevu kwa njia ya mtandao, atatakiwa kufuata hatua zifuatazo:-
- Kujaza fomu kupitia mtandao wa https://lormis.tpf.go.tz/ na kutoa maelezo ya upotevu
- Akisha jaza fomu hiyo atapatiwa ‘control number’
- Baada ya kupatiwa ‘control’ namba atalipia Tsh 500/= kwa njia ya mtandao
- Baada ya kufanya malipo atatakiwa kwenda kituo chochote cha Polisi kwa ajili ya uthibitisho
- Baada ya kukamilisha hatua zote mwombaji ataprinti fomu hiyo kwa wakati wake.
Kwa
kuanzia, mfumo huu wa utoaji wa fomu ya upotevu kwa njia ya mtandao
umeanza kufanya kazi katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani kama
majaribio na ifikapo mwezi Juni, 2019 mfumo huo utatumika nchi nzima.
Jeshi la Polisi nchini linatoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano katika mapambano dhidi ya uhalifu kwa kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu ili kuendelea kudumisha amani na usalama wa nchi yetu.
Imetolewa na:
…………………………………
Ahmed Z. Msangi – DCPJeshi la Polisi nchini linatoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano katika mapambano dhidi ya uhalifu kwa kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu ili kuendelea kudumisha amani na usalama wa nchi yetu.
Imetolewa na:
…………………………………
Msemaji wa Jeshi la Polisi
Makao Makuu ya Polisi.
0 Comments